Browse images and videos on Instagram. Find out Most Popular Hashtags and Users.Picgra
  1. Homepage
  2. itaendelea

#itaendelea hashtag

Posts attached with hashtag: #itaendelea

Advertisement

Shaaban Habibu🇹🇿🇰🇪🌹 (@storynzuriiplanet) Instagram Profile Photostorynzuriiplanet

Shaaban Habibu🇹🇿🇰🇪🌹

 Instagram Image by Shaaban Habibu🇹🇿🇰🇪🌹 (@storynzuriiplanet) with caption : "MUME WANGU -03

Siku mbili baada ya kuanza zamu ya usiku kazini, nilihisi kukosa utulivu na nilikuwa nikimpigia simu mum" at Dar es Salaam, Tanzania - 2004265369809021168

MUME WANGU -03 Siku mbili baada ya kuanza zamu ya usiku kazini, nilihisi kukosa utulivu na nilikuwa nikimpigia simu mume wangu mara kwa mara na kumuuliza kama yuko salama. Mume wangu aliniambia kuwa kila kitu kipo shwari na yeye yuko salama, hivyo sikuwa na wasiwasi kuhusu chochote. Saa moja baadaye usiku wa manane, nilipata ujumbe wa simu kutoka kwa mume wangu akiniambia: “Belinda alikuja chumbani kwetu akiwa mtupu na kutaka nifanye nae mapenzi”. Nilihisi kama nataka kuanguka, nikawa na maswali mengi kichwani, itakuwaje kama kweli alifanya, na sasa anataka kujisafisha na kujionesha kuwa ni mwanaume mwema? Ni wanaume wachache sana wanaoweza kukataa ofa yenye majaribu kutoka kwa msichana mzuri na mrembo. Baada tu ya kumaliza kusoma ujumbe wa mume wangu, nilipokea ujumbe mwingine kutoka kwa Belinda akisema kuwa kuna kitu muhimu anataka kuniambia. Usiku ule ulikuwa mrefu kwangu, sikuweza kuweka nguvu kwenye mambo mengine. Ilipofika saa 10 alfajiri, niliomba ruhusa na nilidanganya kuwa mwanangu anaumwa, hivyo nilihitaji kuondoka mapema. Nilipewa ruhusa nilipofika nyumbani Belinda alianza kulia akisema kuwa hajui kilichomtokea na kwamba ana hofu sana. Aliponieleza, ndipo nilipoamini kuwa mume wangu alikuwa akisema ukweli. Nilipoingia chumbani kwetu mume wangu alinyanyua na tukakumbatiana kwa dakika kadhaa. Nilijivunia sana kuwa nae na kuona kuwa mimi ni mwanamke mwenye bahati, ilikuwa ajabu sana. Nilichanganyikiwa mno kwa sababu Belinda ni mpwa wangu ambaye nilimpenda sana. Ni binti wa marehemu kaka yangu na niliahidi kumlea mpaka atakapoweza kujitegemea, sasa nilifanya kosa gani kumchukua? Nikimfukuza nyumbani, ataenda wapi? Sijui mama yake mzazi alipo, nitafanyaje sasa? #ITAENDELEA

Advertisement

Shaaban Habibu🇹🇿🇰🇪🌹 (@storynzuriiplanet) Instagram Profile Photostorynzuriiplanet

Shaaban Habibu🇹🇿🇰🇪🌹

 Instagram Image by Shaaban Habibu🇹🇿🇰🇪🌹 (@storynzuriiplanet) with caption : "MUME WANGU-02

Mwaka mmoja na nusu tulikuwa katika maelewano mazuri, lakini baada ya kujifungua mtoto wa 3, Belinda alia" at Dar es Salaam, Tanzania - 2003814613435831199

MUME WANGU-02 Mwaka mmoja na nusu tulikuwa katika maelewano mazuri, lakini baada ya kujifungua mtoto wa 3, Belinda alianza kubadilika. Ushauri wangu kwake haukuwa na maana yoyote, alimsikiliza Moses tu. Alikuwa akinitazama na kusema kuwa mimi ni mnene sana na kwamba wanaume wanapenda wanawake wembamba kama yeye. Mwanzoni ilionekana kama utani tu lakini baadaye ikawa kama mazoea. Nilikuwa nikimwambia kuwa wanaume wanatofautiana katika uchaguzi wao na pia mimi sikuwa mnene sana kama alivyokuwa akiongeza chumvi. Siku moja tulikuwa tukitazama mashindano fulani kwenye televisheni, akaanza kucheka kwa sauti kubwa huku akinyoosha kidole kwa mmoja wa washiriki wa mashindano na kusema: “Shangazi Faith, usipoangalia uzito wako utaishia kuwa kama yule”. Mwanamke aliyemuelezea alikuwa na kilo 442, nami nilikuwa na kilo 60. Hapo mume wangu akaonekana kusononeka na kumwambia kuwa nilikuwa na uzito sahihi na mzuri hata kama nina watoto 3 na akamuonya asirudie kuzungumza nami kwa namna ile… Ukweli mimi sikuchukulia kuwa ni tusi kwa sababu alikuwa mtu wa karibu mno kwangu, lakini mume wangu aliposema vile, akawa kama amenifungua macho. Siku zilivyozidi kusonga mbele, nilibaini kuwa Belinda ni binti mtata na ni kumridhisha. Alitaka vitu vingi, sikushangaa kwamba ilikuwa vigumu kwake kuishi na mama yake wa kambo, ambaye alikuwa mwanamke mzuri na mwema. Jioni moja ya Jumapili kabla sijaanza zamu ya usiku kazini kwangu, alianza kuniambia kuwa mimi ni mwanamke mzuri na kwamba nina bahati sana kuolewa na mwanaume kama Moses. Alinieleza waziwazi kwamba angependa kupata mume kama yeye. Jioni ile nilishawishika kuamini kwamba alikuwa akimtaka mume wangu lakini nilimwambia kuwa anatakiwa kuweka macho yake kwenye masomo, Mungu atampa anayoyatamani! Nilishindwa kukaa nalo, nilimpigia simu Hamasa na kumwambia kuhusu jambo hilo. Alinishauri niwe makini sana na Belinda. Siku mbili baada ya kuanza zamu ya usiku kazini, nilihisi kukosa utulivu na nilikuwa nikimpigia simu mume wangu mara kwa mara na kumuuliza kama yuko salama. #ITAENDELEA

Advertisement

Shaaban Habibu🇹🇿🇰🇪🌹 (@storynzuriiplanet) Instagram Profile Photostorynzuriiplanet

Shaaban Habibu🇹🇿🇰🇪🌹

 Instagram Image by Shaaban Habibu🇹🇿🇰🇪🌹 (@storynzuriiplanet) with caption : "MUME WANGU 01

Baba yangu alifariki dunia nilipokuwa darasa la 3. Ni siku ambayo ilibadilisha maisha yetu kutoka kwenye " at Dar es Salaam, Tanzania - 2003810700267717547

MUME WANGU 01 Baba yangu alifariki dunia nilipokuwa darasa la 3. Ni siku ambayo ilibadilisha maisha yetu kutoka kwenye hali nzuri kwenda kwenye hali mbaya. Mama yangu alikuwa mama wa nyumbani na alitegemea moja kwa moja kipato cha baba yetu. Kuanzia hapo, mama yangu akachukua jukumu la matunzo yangu na kaka yangu mkubwa George. Ndugu wa baba yangu walichukua mali zetu zote ikiwemo nyumba tuliyokuwa tukiishi. Baada ya miaka miwili ya tabu na mateso, hatimaye mama yangu alipata kazi kama mfanya usafi kwenye eneo ambalo baba yangu alikuwa akifanya kazi. Nilipofika darasa la 7 na kaka yangu akawa amefika chuo, mama yetu kipenzi alifariki dunia. Hakuna aliyekuwa tayari kutuchukua mimi na mtoto wa kaka yangu, Belinda aliyekuwa na umri wa miaka 4. George alipata mtoto nje ya ndoa alipokuwa kidato cha 3, mwaka mmoja baada ya kifo cha baba yangu. Mama ndiye aliyekuwa akimhudumia mtoto huyo tangu alipozaliwa. Mungu ni mkubwa, rafiki mkubwa wa mama yangu kutoka kanisani, Jessica alituchukua. Alikuwa mjane mwenye mtoto mmoja tu. Binti yake, Hamasa na mimi tulikuwa kama mtu na dada yake, hivyo tulipendana sana. Shangazi Jessica alikuwa mtu mzuri na mwema, alituhudumia kama watoto zake halisi. Kaka yangu alikuwa akija siku za likizo mpaka alipohitimu masomo yake. Nilichagua kusomea uuguzi baada ya kuhitimu masomo yangu ya kidato cha sita kwa sababu nilitaka kuchukua kozi ambayo itakuwa rahisi kupata kazi. Nikiwa mwaka wa mwisho chuoni, nilikutana na mume wangu Moses na tulifunga ndoa baada ya mwaka mmoja na nusu wa mahusiano yetu… Baada ya kujifungua mtoto wangu wa pili, kaka yangu George alifariki dunia katika ajali ya gari. Hakika nilichanganyikiwa sana. Mimi na kaka yangu tulipendana sana na tulielewana mno. Aliacha mke na watoto wanne. Belinda hakuweza kuwa na maelewano mazuri na mama yake wa kambo, hivyo nilimchukua. Sikutaka apate usumbufu kwenye masomo yake. Wakati huo alikuwa kidato cha 3 na niliamini kuwa atafaulu vizuri sana. Mwaka mmoja na nusu tulikuwa katika maelewano mazuri, lakini baada ya kujifungua mtoto wa 3, Belinda alianza kubadilika. #ITAENDELEA

Shaaban Habibu🇹🇿🇰🇪🌹 (@storynzuriiplanet) Instagram Profile Photostorynzuriiplanet

Shaaban Habibu🇹🇿🇰🇪🌹

 Instagram Image by Shaaban Habibu🇹🇿🇰🇪🌹 (@storynzuriiplanet) with caption : "SALHA 47

Nikiwa sielewi. Nikiwa nimechanganyikiwa. Niifanye ile kazi ama la. Na dau lilikuwa limepanda, milioni thelath" at Dar es Salaam, Tanzania - 2002238369456078206

SALHA 47 Nikiwa sielewi. Nikiwa nimechanganyikiwa. Niifanye ile kazi ama la. Na dau lilikuwa limepanda, milioni thelathini zaidi juu ya zile ishirini alizonambia Bizzo. "Hapa nishaingia choo cha kike. Nilikuwa na uwezo wa kumkatalia Bizzo kabla, lakini sio watu hawa wasioeleweka" Niliwaza kimoyomoyo. Nikajipa moyo "Nayafanya haya yote kwa ajili ya maisha yangu na Salha. Mwanamke ninayempenda kuliko kitu chochote kile. Wacha niende niko tayari kwa lolote, na hii ni kwaajili yako Salha.." Niliinama na kuichukua ile 'brief case' nyeusi. Nilisikia majamaa wote watatu wakipiga makofi ya kunipongeza. Nilitoka nje ya chumba namba nane ndani ya nyumba ya kulala wageni ya Machenza na kuelekea shule ya msingi Stadium, nikiwa na begi langu mkononi, nilipita katika kichochoro kirefu ili kutokea katika njia itakayonipeleka moja kwa moja katika barabara itakayoweza kunifikisha shule ya msingi Stadium. Niliumaliza uchochoro. Nilipofika tu barabarani, mbele ya miguu yangu lilikuwa limesimama gari ndogo ya Polisi huku ikipiga ving'ora kwa fujo. Harakaharaka walishuka askari wanne wakiwa na bunduki mkononi. Zote zilielekezwa kwangu. Nilisimama wima nikiwa na 'brief case' yangu mkononi. Nilichanganyikiwa sana. Ulikuwa wakati wa mashaka kuliko wakati wowote katika maisha yangu. Ulikuwa wakati wa uwoga kuliko wakati wowote katika maisha yangu. Uwoga wa kiwango cha juu. Nilitetemeka haijawahi kutokea hapa duniani. Nilitetemeka vibaya mno. Sikuwa na kosa lolote. Lakini sikujua ni kitu gani kilichokuwemo ndani ya 'brief case' iliyokuwepo mikononi mwangu. Polisi walianza kunisogelea kwa hatua za taratibu. Midomo ya bunduki zao zote zikielekezwa katikati ya kifua changu. Sikuweza kuvumilia, sikuweza katu...Niliyahisi majimaji mepesi ya moto yakitiririka mapajani mwangu, mkojo ulinitoka bila kupenda. Nilijikojolea. Askari mmoja alinizunguka kwa nyuma. Mkono wa kulia akiwa kashika bunduki kubwa, kwa kutumia mkono wa kushoto alinikwida suruali yangu na kuninyanyua juujuu. Nilikuwa natembelea vidole. Nilitembezwa kuelekea garini, nilipokaribia gari alinibeba msobemsobe na kuniingiza garini. #ITAENDELEA

Vennita Mwita (@vennita_mwita) Instagram Profile Photovennita_mwita

Vennita Mwita

 image by Vennita Mwita (@vennita_mwita) with caption : "#Kosa_langu  #Hadithi_inaendelea 
#Sehemu_15 #Mtunzi @vennita_mwita ..."Mambo vipi washikaji, naweza lala hapa pia?" Nil" - 2001819767496958372
ReportShareDownload043

@vennita_mwita ..."Mambo vipi washikaji, naweza lala hapa pia?" Niliwauliza. "Wewe nani na umetoka mtaa gaini?" aliniuliza mmoja wao aliyeonekana kuwa mkubwa zaidi. Sikuficha kitu,nilieleza yote,uyatima, safari, na jinsi nilivyofukuzwa na polisi. Lengo langu la kufika Ileje. Walinihurumia yatima mwenzao,lakini kuu zaidi na furaha yangu ilitimia pale waliponiambia wanapafahau kwa mjomba wangu,yaani Mwalongo Namela Mwabuka kwani ni diwani wa ile kata! Sikutaka kusubiri asubuhi ifike, niliwaomba wanipeleke muda huo huo! Walikubali! Nilifurahi san asana! Tulienda mpaka hapo, sikuijua hata sura yake,lakini nilitumaini atanipokea. Tulifika na kugonga mlango, baada ya kugonga sana,alifungua kijana," mnataka nini, kwanini mnatusumbua kwenye starehe zetu, hamjui tunasoma kesho tunamtihani, nyie machokoraa vipi,au mmeambiwa hapa kituo cha polisi au kanisa la misaada? Semeni haraka mnachotaka, lakini pesa au chakula hakuna!" alifoka. "Samahani, tumewaletea Mgeni wenu," alisema mmoja wetu. Nami nilijieleza. Cha ajabu yule kijana alicheka sana," hizo ndio mbinu zenu ee? Ngonja niwaitie bi mkubwa," (yaani mama yake).Baada ya muda alitoka mama mnene sana, kakunja uso, hakuipokea hata salam yetu! Nilijieleza tena na kuomba kuonana na mjomba wangu, walau nimuone tu sura yake. Umalaya, ukahaba na umasikini wa mama yako usitupe shida wengine umesikia eeeh?! Mjomba wako hakumtuma akazae hovyo kama mbwa, OK? Umefikaje hapa? Umeona sie wapuuzi kama wewe? Unadhani hatujui mbinu zenu mpya za wizi siku hizi etii?! Sikuhitaji ondoka kwani nyumba yangu imejaa, katafute msaada katika vituo vya watoto yatima! Akaniachia msonyo mkubwa ambao sijawahi kuusikia tangu nizaliwe! Nililia,niliziba masikio sikutaka kusikia zaidi, sikuwa tayari kuamini, mimi sio mwiziiii! Mimi ni Paulooooo! kwa mara ya kwanza nilipatwa na hasira kali,nilimsukume yule mama nikaingia ndani na kupiga kelele mfululizo, "mjomba uko wapi? Njoo uniulie kwako kama kweli hamnitaki, njoo mjomba popote ulipo! Njoo uniue mpwa wako!" nilitamka haya maneno pasipo na idadi. Alitoka pande la mwanaume, "ndio wewe Mwalongo....? #Itaendelea..

Shaaban Habibu🇹🇿🇰🇪🌹 (@storynzuriiplanet) Instagram Profile Photostorynzuriiplanet

Shaaban Habibu🇹🇿🇰🇪🌹

 image by Shaaban Habibu🇹🇿🇰🇪🌹 (@storynzuriiplanet) with caption : "SALHA 44

Niliangalia saa yangu aina ya Adam Kimmel original. 
Ilikuwa ni saa tano na nusu usiku. 
Nusu saa kabla ya mud" - 2001473176136508895
ReportShareDownload053

SALHA 44 Niliangalia saa yangu aina ya Adam Kimmel original. Ilikuwa ni saa tano na nusu usiku. Nusu saa kabla ya muda wa miadi yetu. Nilimuacha Salha, nikatokomea gizani. Nilisikia kilio cha kwikwi toka kwa Salha. Sikugeuka nyuma. Nilijua nikigeuka nyuma nisingeweza kuondoka. Nilikuwa naenda, naenda kutafuta pesa. Na ilinipasa niende kabla saa sita usiku haijafika. Saa tano na dakika hamsini usiku ilinikuta nikiwa nje ya nyumba ya kulala wageni ya Machenza, kibao cha bluu kilikuwa kinaninginia mlangoni kiliandikwa…Machenza Guest House. Kwa mwendo wa taratibu, kama nilikuwa nalazimishwa na mtu nilienda hadi mapokezi. Nilikutana na dada mmoja akimhudumia mteja. Nilisimama wima nikisubiri zamu yangu ifike. Baada ya kuyaandika maelezo ya yule jamaa kwenye kitabu cha wateja. Alimuelekeza chumba yule mteja, hapo nami nililisogelea dirisha. Baada ya salamu nilimueleza maelezo aliyonipa mwenyeji wangu niyaseme kwake. Na nilimtajia hadi namba ya chumba alichokuwemo mwenyeji wangu. Chumba namba nane. Chumba alichokuwa amepanga kijana niliyekuwa namfahamu kwa jina moja tu, Bizzo. Mhudumu alinielewa, aliniamini, aliniruhusu niende chumba namba nane huku akinionesha mahali kilipo chumba hicho kwa mkono. Bila shaka Bizzo aliacha salamu kwamba atakuwa na mgeni kama alivyoniambia. Nilitembea taratibu sana kuelekea chumba namba nane. Nilitembea huku mawazo lukuki yakikitawala kichwa changu. "Pole sana kwa yote yaliyokukuta Dokta. Na nakwambia hauwezi kuishi kwa raha Bongo kwa hiko kisanga kilichokukuta mshkaji wangu. Cha msingi na cha sekondari hapo ni kusepa nje. Kajichimbie Bondeni huko ama hata Malawi na huyu mtoto mzuri, haya mambo yakipoa utarejea tena Bongo.." Niliikumbuka sauti ya Bizzo ikivyonambia ndani ya gari. Wakati huo Salha akiwa kajilaza magotini kwangu. Nakumbuka nilimuuliza "Sasa mimi nitapata wapi pesa za kuweza kunifikisha South Africa au huko Malawi Bizzo? Yatakiwa niwe na pesa za kutosha ili nisiende kugeuka ombaomba katika nchi za watu" We’ ni mwanaume. Ukifanya mishe utapata mpunga wa kukufikisha huko. Sasa sikia mshkaji wangu, njoo Machenza Guest house saa sita kamili usiku. #ITAENDELEA

Shaaban Habibu🇹🇿🇰🇪🌹 (@storynzuriiplanet) Instagram Profile Photostorynzuriiplanet

Shaaban Habibu🇹🇿🇰🇪🌹

 Instagram Image by Shaaban Habibu🇹🇿🇰🇪🌹 (@storynzuriiplanet) with caption : "SALHA 43 " Unaenda wapi Muu usiku huu?" Nilimjibu kwa upole "Naenda kutafuta Salha, kutafuta ili tuweze kuishi kesho, tu" at Dar es Salaam, Tanzania - 2000868206219600345

SALHA 43 " Unaenda wapi Muu usiku huu?" Nilimjibu kwa upole "Naenda kutafuta Salha, kutafuta ili tuweze kuishi kesho, tuweze kuishi na kesho kutwa. Lazima tuendelee kuishi Salha ili kutimiza ndoto zetu, na ili tuishi lazima tule mpenzi. Hatuwezi kula bila kuwa na pesa. Naenda kutafuta pesa mpenzi, na.." Salha alinikata kauli "Kutafuta pesa usiku huu Muu?" Salha aliniuliza huku akiinuka. "Wapi utapata pesa usiku huu. Sahivi ni usiku, saa tano usiku. Utaenda kufanya nini ili upate pesa Muu. Tulale, kesho asubuhi tutajua nini cha kufanya" Nilisema tena kwa sauti ya kusisitiza. "Kesho maisha hayaanzi Salha, kesho maisha yataendelea. Lazima tuwe na fedha za kuweza kutuwezesha kuendelea na maisha. Lazima nikasake pesa na nina hakika nitazipata usiku huu. Nakuahidi nitarudi hapa kabla ya saa saba usiku" Niliongea huku nikinyanyuka. Salha nae alinyanyuka. Alinisogelea. Alinikumbatia kwa nguvu. Akanipiga busu katikati ya paji langu la uso. Akanipiga busu tena katika shavu langu la kulia. Akanipiga busu lengine katika shavu langu la kushoto. Akanibusu mdomoni. Midomo yetu iligandana kwa muda. Alitoa ulimi wake. Nikaupokea vizuri kwa ulimi wangu. Nilinyonya ulimi wa Salha. Niliunyonya ulimi mtamu sana kama asali. Tulitumia dakika kumi tukiwa katika hali hiyo. Tukipeana denda. Lilikuwa denda refu zaidi kuwahi kupiga hapa duniani. Tukaachiana. Tuliangaliana usoni. Salha alikuwa analia. Mimi halikadhalika nilikuwa ninalia. "Nakupenda sana Muu", alisema kwa sauti yake nyororo "Nakupenda zaidi Salha" nilimjibu “…nakuahidi nitakupenda siku zote za maisha yangu. Wewe ni shujaa kwangu. Shujaa wangu, shujaa wa kweli. Hakuna mwanaume kama wewe Muu. Wewe ni mwanaume bora sana katika zama hizi. Zama za wanaume wasaliti. Kwangu, wewe ni mwanaume wa pekee sana. Kama kuna mwanamke mwenye bahati basi ni mwanamke anayeishi na wewe Muu, . Na Salha nimeipata hiyo bahati. Sipo tayari kuipoteza hata kitokee nini, alisema Salha." Nilimziba mdomo Salha. Machozi yalikuwa yanambubujika kwa wingi. Nilimuonea huruma sana. Kumuona mwanamke niliyempenda zaidi akilia. Iliniuma sana. Niliangalia saa yangu aina ya Adam Kimmel original. Ilikuwa ni saa tano na nusu usiku. #ITAENDELEA

Shaaban Habibu🇹🇿🇰🇪🌹 (@storynzuriiplanet) Instagram Profile Photostorynzuriiplanet

Shaaban Habibu🇹🇿🇰🇪🌹

 Instagram Image by Shaaban Habibu🇹🇿🇰🇪🌹 (@storynzuriiplanet) with caption : "SALHA 42

Baada ya kutembea kama robo saa kutokea kijiji cha Hoteli tau tuliomba lifti katika lori, lori lililotufikisha" at Dar es Salaam, Tanzania - 2000866406485482182

SALHA 42 Baada ya kutembea kama robo saa kutokea kijiji cha Hoteli tau tuliomba lifti katika lori, lori lililotufikisha katika mji wa Lindi saa mbili usiku. Tulijisikia huru kuwa mbali na wakina Vampire, lakini tulipofikiria maisha yetu yataenda vipi ndani ya Lindi ulitupata woga mkuu. Usiku huo tulipanga kulala katika stendi ya Lindi. Laiti ningejua madhila ya usiku huo haki ya Mungu tusingepanga kulala stendi ya mabasi..au pengine nisingeenda Lindi kabisa. Tulikaa katika kibaraza cha duka moja katika stendi ya mkoa wa Lindi hadi saa tano usiku. Salha alidai amechoka sana. Alikuwa anahitaji kupumzika. Nilitandika maboksi machache mbele ya kile kibaraza cha duka. Nilikaa chini nikiwa nimenyoosha miguu yangu yote miwili. Salha alilala katika miguu yangu. Hazikufika hata dakika sita, Salha alikuwa anakoroma. Sikutaka kukaa mahali pale. Mimi ndiye nilikuwa mwanaume, nilikuwa tegemezi. Ilinipasa kutafuta namna sahihi ya kuona kesho yetu inakuwaje. Nilimuinua Salha taratibu akiwa usingizini, nikamlaza chini ya boksi. Nilimwangalia. Nikainama. Nilikuwa naiangalia sura nzuri sana ya Salha. Ilikuwa imelala kitulivu sana. Sura nzuri, sura nzuri ya mwanamke wa maisha yangu. Nilisogeza mdomo wangu karibu na mdomo wake. Nikambusu. Nilisema kwa sauti ndogo sana "Nakupenda sana Salha. Nakuacha hapa mpenzi lakini nitarudi. Naenda kutafuta baby, nitarudi muda si mrefu” Nilisema kwa sauti kubwa kidogo, karibu na sikio la Salha “…nakuahidi mpenzi, nitakupenda siku zote za maisha yangu. Nitakupenda milele. Nitakupenda kwa kuwa nimeamua kukupenda. Nimekupa moyo wangu Salha. Moyo wangu wote. Nipo tayari kuwa na wewe katika nyakati zote, nyakati za shida kama hizi, nyakati za raha. Amini upo na mtu sahihi, mtu atakayekupigania katika nyakati zote za maisha. Sitothubutu kukuacha peke yako Salha, Sitokutesa hata sekunde moja mpenzi wangu. Siwezi kabisa kumtesa mwanamke ninayempenda sana hapa duni.." Sikumalizia kuongea. Niliona machozi yakitiririka katika mashavu ya Salha. Kumbe alikuwa ananisikia. Alifumbua macho. Tuliangaliana. Alisema kwa sauti ya kwikwi " Unaenda wapi Muu usiku huu?" Nilimjibu kwa upole "Naenda kutafuta Salha, #ITAENDELEA