Browse images and videos on Instagram. Find out Most Popular Hashtags and Users.Picgra
  1. Homepage
  2. @storynzuriiplanet
Shaaban Habibu🇹🇿🇰🇪🌹 (@storynzuriiplanet) Instagram Profile Photo storynzuriiplanet
Fullname

Shaaban Habibu🇹🇿🇰🇪🌹

Bio 🔵East African Artist 🔥Mr Romantic TANZANIANBOY🇹🇿 Subscribe YouTube channel (storynzuriiplanet) 👇👇👇👇👇

Profile Url

Share
Statistics for "Shaaban Habibu🇹🇿🇰🇪🌹 (@storynzuriiplanet)"
Suggested users for Instagram Profile "Shaaban Habibu🇹🇿🇰🇪🌹 (@storynzuriiplanet)"
Wema Sepetu (@wemasepetu) Instagram Profile Photowemasepetu

Wema Sepetu

Chibu  Dangote..! (@diamondplatnumz) Instagram Profile Photodiamondplatnumz

Chibu Dangote..!

Irene Uwoya (@ireneuwoya8) Instagram Profile Photoireneuwoya8

Irene Uwoya

Idris Sultan (@idrissultan) Instagram Profile Photoidrissultan

Idris Sultan

C H U M A (@rayvanny) Instagram Profile Photorayvanny

C H U M A

Shaaban Habibu🇹🇿🇰🇪🌹 (@storynzuriiplanet) Instagram photos and videos

List of Instagram medias taken by Shaaban Habibu🇹🇿🇰🇪🌹 (@storynzuriiplanet)

Advertisement

 Instagram Image by Shaaban Habibu🇹🇿🇰🇪🌹 (@storynzuriiplanet) with caption : "PART 2 "Tumuache binti yetu aamue, nenda na ukamkaribishe Mzee UPENDO kama binti yetu alivyopendekeza" Mume aliongea.

M" at Dar es Salaam, Tanzania - 1979928801778757448

PART 2 "Tumuache binti yetu aamue, nenda na ukamkaribishe Mzee UPENDO kama binti yetu alivyopendekeza" Mume aliongea. Mke alitoka nje na kuwauliza wale wazee watatu, "Mlisema ni nani kati yenu anaitwa Mzee UPENDO? Tafadhali sana karibu nyumbani kwetu na uwe mgeni wetu." Mzee UPENDO akanyanyuka na kuanza kufuatana na yule mwanamke. Wale wazee wawili waliobaki nao wakaanza kufuata nyuma. Kwa mshangao yule mwanamke akauliza nimemualika Mzee Upendo tu, na ninyi ndivyo mlovyosema kwamba hamuwezi kuingia wote, sasa iwaje nanyi wawili mnakuja ndani? Wazee wote watatu kwa pamoja wakajibu: "kama ungalikuwa umemualika kati ya UTAJIRI au MAFANIKIO, wawili tungalibaki nje, ila kwa kuwa umemualika UPENDO popote atakapoenda sisi tutamfuata. Baada ya Upendo kuingia ndani ya nyumba, upendo ulitamalaki ktk familia, amani ya roho ikawepo, utajiri ukajisogeza zaidi na mafanikio wakayapata. 💑💑 Popote penye upendo kuna utajiri na mafanikio. Upendo ni dhana pana sana Paulo anasema, "Tena nikitoa mali zangu zote kuwalisha maskini, tena nikijitoa mwili wangu niungue moto, kama sina upendo, hainisaidii kitu. Upendo huvumilia, hufadhili; upendo hauhusudu; upendo hautakabari; haujivuni; haukosi kuwa na adabu; hautafuti mambo yake; hauoni uchungu; hauhesabu mabaya; Haufurahii udhalimu, bali hufurahi pamoja na kweli; Huvumilia yote; huamini yote; hutumaini yote; hustahimili yote." Mwenyezi Mungu atuongoze ili Upendo, utajiri na mafanikio viwe na sisi daima UPENDO NI TIBA . NAWAPENDA 💟💞💖 STORY HII KWA UDHAMINI WA @CITYSWEETESTJUICE ANAPATIKANA MTONGANI KWA AZIZI ALLY MCHEK KWA ORDER ZA JUICE BEI SAWA NA BURE @CITYSWEETESTJUICE@CITYSWEETESTJUICE@CITYSWEETESTJUICE

Advertisement

 Instagram Image by Shaaban Habibu🇹🇿🇰🇪🌹 (@storynzuriiplanet) with caption : "Karibu saana @citysweetestjuice Kwa juice tamu zenye ladha maridhawa anapatikana mtongani kwa Azizi Ally....... SHORT ST" at Dar es Salaam, Tanzania - 1979926402477444731

Karibu saana @citysweetestjuice Kwa juice tamu zenye ladha maridhawa anapatikana mtongani kwa Azizi Ally....... SHORT STORY Siku moja mwanamke alitoka nje ya nyumba na kuwaona wazee watatu wenye mvi kichwani wakiwa wamekaa nje ya nyumba yake. Hakuwatambua na wala hakuwa anawafahamu. Akawaambia, "nafikiri siwafahamu, ila inavoonesha mna njaa sana. Tafadhali wazee wangu mkaribie nyumbani kwangu japo mpate hata chakula" "Baba mwenye nyumba yupo?", mmoja wa wale wazee aliuliza. "Hapana" yule mwanamke alijibu "Ametoka kidogo." "Basi hatuwezi kuingia ndani", wale wazee walimjibu. Jioni mume wake aliporudi, mke alimueleza kilichotokea. "ah wale wazee watatu nami nimewaona hapo nje ila sikutaka kuwatilia maanani, nenda kawaambie nimerudi na wakaribishe ndani" Mume alimwambia mkewe. "Hatuwezi kuingia ndani ya nyumba yenu sisi sote", wazee walijibu baada ya mke kuwaambia kwamba mumewe amerudi na anawahitaji. "Kwanini?" mke alitaka kujua. Mmoja wa wale wazee akamuelezea: "Huyu mwenzangu (huku akimshika bega mzee mwenzake) anaitwa UTAJIRI, na huyu mwingine (huku akimnyoshea kidole) anaitwa MAFANIKIO na mimi ninaitwa UPENDO." baada ya kujitambulisha yule mzee akamwambia yule mwanamke, "sasa nenda ndani ukajadiliane na mume wako nani kati yetu aingie ndani ya nyumba yenu, yaani Utajiri, Mafanikio au Upendo" Mwanamke akaingia ndani na kumueleza mume wake yale aliyoambiwa na Mzee upendo. Mume wake alifurahi sana. Akasema, "vizuri sana, kwa kua ndio hivyo basi tumkaribishe UTAJIRI aingie ndani ya nyumba yetu, muache aje ndani ya familia yetu na atupe utajiri" Mke hakukubaliana na matakwa ya mume wake. "Mpenzi kwanini tusimkaribishe Mzee MAFANIKIO?" Wakiwa wanaendelea kubishana, binti yao mdogo aliyekuwa akiwasikia wakibishana akaja na mawazo yake, binti akasema: "Je haitakuwa vema tukimkaribisha Mzee UPENDO?, nyumba yetu itajazwa na upendo. Kwa maana humu kila siku imekuwa ugomvi tu, baba na mama mnagombana na kupigana mimi bila kujua sababu." "Tumuache binti yetu aamue, nenda na ukamkaribishe Mzee UPENDO kama binti yetu alivyopendekeza" Mume aliongea.

Advertisement

 image by Shaaban Habibu🇹🇿🇰🇪🌹 (@storynzuriiplanet) with caption : "@pixelspro_films WAMEKUANDALIA OFFER KABAMBE KATIKA KIPINDI HIKI KUELEKEA VALENTINE DAY WANAPATIKANA KIJICHI MCHEKI @rob" - 1978301095299324579
ReportShareDownload11116

@pixelspro_films WAMEKUANDALIA OFFER KABAMBE KATIKA KIPINDI HIKI KUELEKEA VALENTINE DAY WANAPATIKANA KIJICHI MCHEKI @robhinedson@directorsniper@pixelspro_films KWA MAELEKEZO ZAIDI PICHA KALI NA ZA KIBABE NA KIMAHABATI MAHABATANI *Ili uolewe MAPEMA Mdada tumia Mbinu hii* ```Mtafute ndugu yako anaekaa mbali sana na wewe, mfano ni shangazi yako au dada yako.... hamia kwake kimakazi kwa muda, ukifika kwake nenda na tabia zingine mpya, kuwa mkarimu sana, kuwa mpole sana, ipende dini yako na ifuate, wapende wamama watu wazima na wababa, wapende mabibi na mababu, wakarimu sana pia wape misaada midogo midogo, mfano ukimkuta mama naniu bombani msaidie kubeba ndoo yake ya maji, ukikutana na mzee na niniu njiani msaidie kamzigo kake mpaka kwake. Niamini mimi kuwa hawa watu kila mmoja atatamani uwe mkwe wake, pia vijana wa kiume kila atakae kutongoza mkatalie, watatumana kwa fujo kila mmoja kutaka kukufunua ili akatambe kijiweni kuwa yule binti mwenye msimamo mie nimemuweka😋 lakini jaribu kukaza usimkubalie ata mmoja, ikitokea hamu imekushika sana unafunga safar unaenda kule kwenu ulipozaliwa ambako kila mtu anakujua kwa umalaya wako, nenda mtafute bwanaako mpe utamu ajilie vyake mpaka kiu ikuishe, kesho yake unarud tena kwa shangazi, ukifika kule ni mwendo wa kukaza na kukomaa, usimpe mtu. kuanzia hapo sasa utaanza kupata sifa kama za bikira Maria, kila mtu atakuwa anakusifia wewe, kila mwanaume atatamani akuoe wewe. zitaanza kugongana posa kwa shangazi yako, akitoka uyu anaingia uyu, utachagua kwa nafas yako. ukitaka mrefu au mfupi hapo ni wewe tu. tumia iyo mbinu ikishindikana, Nipigie Simu Mimi.```

HAPPY BIRTHDAY TO YOU.

 Instagram Image by Shaaban Habibu🇹🇿🇰🇪🌹 (@storynzuriiplanet) with caption : "NDOA NA TENDO LAKE!
PART 2

Wanaume wajifunze HISIA za wake zao na wanawake wafahamu MUUNDO wa waume wao. 
Tatizo kubwa " at Dar es Salaam, Tanzania - 1977438651983287279

NDOA NA TENDO LAKE! PART 2 Wanaume wajifunze HISIA za wake zao na wanawake wafahamu MUUNDO wa waume wao. Tatizo kubwa kwa wanaume ni kutojua majira ya kujiliwa kwa wanawake na namna ya kuwaandaa wake zao, na hivyo tendo la ndoa linakuwa ubakaji tu! Ipo lugha ya kuongea na mwanamke inayoweza kusaidia kupunguza stress na kumuweka sawa kitendo na sio kukurupuka kama afande anawakurupusha makruta wa JKT. Mahusiano chanya kati ya mume na mke ni jambo muhimu. Epuka kumuona mkeo kama takataka au zuzu. Mtafakari vizuri hata kama kwako anaonekana ana kasoro. Usimdhalilishe mbele ya mtu yeyoooooooooooooote hata kama huyo mtu ni nani kwako! Adamu alimsema vibaya Hawa mbele ya Mungu BABA, usifanye hivyo ni MWIKO. Wanawake pia, msivae manguo mengi, sisi wanaume tunachoka kuwavua nguo zenu. Mnavaa utafikiri mko Rasi ya Kaskazini kwenye barafu, kwa maeskimo...mpaka mtu afikie ngozi yako utafikiri anapanda Mlima Kilimanjaro! Si ungeenda maonyesho. Mwili wa mwanamke ni RAHA, tuachieni raha zetu😠...Tatizo letu wanaume ni macho! Hata mwanamke mchawi akivua nguo sisi wanaume hatuuoni uchawi tunaona Beautiful Lady😍... Kuna utofauti katika uumbaji wetu, wengine wanaweza kutenda mara tatu kwa siku kila siku, wengine mara moja kwa siku, wengine kwa wiki na wengine kwa mwezi...Ndio maana Mungu BABA anastahili kuwakutanisha wanandoa, ukiingia vibaya utajuta! Mwenye uwezo wa kutenda mara tatu akikutana na mwenye kutenda mara moja kwa mwezi...huyo wa mwezi mara moja ATAKUFA! Kila mnapotenda nguvu ya muunganiko wenu (bond) inaongeza. Watu wanotenda mara kwa mara mshikamano wao huwa mkubwa kuliko wasiotenda mara kwa mara. Yako matatizo ya kihomoni, ambapo wenye homoni chini ya kiwango cha kawaida hamu yao ya tendo la ndoa huwa mbali na wenye homoni nyingi hamu ya tendo la ndoa huwa juu. Kwa wanaume pia ipo kwa kiwango kidogo na kwa wanawake ni kubwa. Homoni hubadilisha joto la mwili na husababisha hali ya kutaka kutenda na wakati mwingine usipotenda utaota unatenda na hii sio majini mahaba bali ni baiolojia ya mwili. SASA SIKIENI MSINILETEE ZA KULETA, TENDENI!

 Instagram Image by Shaaban Habibu🇹🇿🇰🇪🌹 (@storynzuriiplanet) with caption : "NDOA NA TENDO LAKE!

Ndoa ni Mahusiano yanayoanza rohoni (wengi hawajui na hawakubali) inatiririkia nafsini (moyoni) na " at Dar es Salaam, Tanzania - 1977437513045134995

NDOA NA TENDO LAKE! Ndoa ni Mahusiano yanayoanza rohoni (wengi hawajui na hawakubali) inatiririkia nafsini (moyoni) na inadhihirika mwilini! Ndoa huanza na wazo (roho+nafsi) baadaye mtu huchukua hatua na kuanzisha mazungumzo. VITABU VYA DINI vinasema, amtazamaye mwanamke kwa macho ya matamanio (mawazo ya moyoni) amekwisha kuzini naye moyoni! Tendo la ndoa linafanywa katika fikra (moyo na roho) kisha mwilini. Nimekutana na watu wengi wanaosema, mwenzi wangu aklwa mbali nam-miss sana lakini akija ile hali inaondoka! Ulimwengu wa giza unahusika sana katika kuvuruga mahusiano ya wanadamu hasa kupitia mapepo wachafu. Mara nyingi unapoota kuwa una ndoa, hiyo ndoa ni ya rohoni; yaani roho yako ina mkataba na roho nyingine... Ndio ile ya jini mahaba. Majini mahaba yanakamata jinsia zote mbili. Nikiwa nafanya huduma, baba mmoja alikuwa na jini jike ambalo lilikuwa linapambana na mke halali wa huyo baba. Mke alikuwa akiota anapigana na mwanamke na liliwazuia wasipate watoto kwani kila baba akimtaka mke wake, anaugua ugonjwa ambao hata hawezi kufanya chochote. Huyu baba yuko huru sasa na wamepata watoto wawili kwa muda wa miaka minne sasa. Kwa wanandoa ambao wako huru, tendo la ndoa ni muhimu sana likafanywa kila wakati. Soma ramani ya mahusiano yenu na tengeneza mazingira sahihi. Wanaume wajifunze HISIA za wake zao na wanawake wafahamu MUUNDO wa waume wao. WAIT FOR PART 2

 Instagram Image by Shaaban Habibu🇹🇿🇰🇪🌹 (@storynzuriiplanet) with caption : "Me nadhani niseme neno moja kwa wanaume wenzangu siku ya leo, ila sijamtaja mtu na kama ikikugusa niombee kwa Mungu, ili" at Dar es Salaam, Tanzania - 1977007491843025912

Me nadhani niseme neno moja kwa wanaume wenzangu siku ya leo, ila sijamtaja mtu na kama ikikugusa niombee kwa Mungu, ili niendelee kukubariki. Ila kama unajua una date na binti wa umri wa kuanzia miaka 23 kuendelea na hauna mpango wa kumuoa fanya jambo la kiungwanana kumuambia ukweli. Sikuambii umuambie kuwa humtaki na hutaki kuoa bali muambie kuwa wewe si muoaji na unaona kama utampotezea muda wake bure na kuja kumuumiza. Ongea kiungwana na ikishindikana muache hata kibabe. Hii ni kwasababu mwanamke anawekeza vitu vingi katika mahusiano, anawekeza akili yake, mali zake, hisia na kubwa kabisa anawekeza umri wake katika mahusiano. Unampunguzia uwezekano wa kukutana na mtu sahihi kwa kuendelea kumdanganya. Kwa Mwanamke, Age is not just a Number Age is Everything. Wakati ukimuacha wewe utatafuta binti mdogo zaidi yake, yeye atalazimika kutafuta Kijana mwenye Umri Mkubwa zaidi yake. Ndiyo ilivyo, sote, Wanaume na Wanawake huangalia Umri katika Mahusiano. Ukimchezea na kumuacha akiwa katika Umri wa Miaka 30, ina maana atafute kijana mwenye Umri kuanzia Miaka 32 ambaye bado yuko Single. Wako wachache sana wa namna hiyo, sisemi kuwa hawezi kupata, hapana, bali nasema utampa wakati mgumu na uhuru wa kuchagua. Kuna umri ambao mabinti wengi huamua kuolewa tu, si kwasababu ya mapenzi bali kwakua hawana namna wanaona kusubiri mtu sahihi watapishana na kalenda. Badilika, haikufanyi Mwanaume zaidi kwa kumpotezea Binti wa watu Miaka Mitano halafu unamuambia "wewe si Type yangu" Fanya jambo la kiungwana na malizaneni mapema, lakini najua kuna Mabinti ambao hawasikii wakiambiwa kuwa mambo yameisha, Mlazimishe asikie na Usimtumie na kumuumiza kwa kuwa anakupenda. Women have many possibilities from 18 to 24 years, but from 25 and above, the graph starts to fall down whether they like it or not. Na wapendwa dada zangu, niwakumbushe tu jambo moja tu nikiwa namaliza "Sisi wanaume asilimia kubwa tukimpenda mwanamke huwa tunapenda kwa sababu maalum. Hivyo mnisamehe wote nilio haribu plan zenu na mwenyezi Mungu awabariki wote mlioacha kazi zenu na kusoma ujumbe huu.

 Instagram Image by Shaaban Habibu🇹🇿🇰🇪🌹 (@storynzuriiplanet) with caption : "HADITHI:MREMBO LATIFA (MWISHOOO)
MTUNZI:EDO MAN  Kwa Ibrahim, japokuwa alimfanyia mambo mabaya nyuma hakutaka kumuacha h" at Dar es Salaam, Tanzania - 1975972957558980823

HADITHI:MREMBO LATIFA (MWISHOOO) MTUNZI:EDO MAN Kwa Ibrahim, japokuwa alimfanyia mambo mabaya nyuma hakutaka kumuacha hivihivi, aliamua kumsaidia kama alivyomsaidia baba yake. Akamnunulia nyumba kubwa Mbezi Beach na kumgawia kiasi cha shilingi milioni mia tatu kwa ajili ya kufanya biashara zake kitu ambacho kwa Ibrahim kilikuwa kitu kikubwa, baada ya wiki moja, akaamua kumpa talaka Nusrat na kumuoa mwanamke mwingine na kuishi naye nyumbani kwake huku akifungua biashara kubwa. Kwa Latifa, akaamua kufunga ndoa ya kishria Dominick na watu hao kuishi pamoja kwa amani ni na upendo ambapo baada ya miaka miwili, wakafanikiwa kupata mtoto wa kiume waliyemuita kwa jina la Godlove. Dawa yake ya kansa ya Morphimousis iliendelea kutikisa duniani, watu waliokuwa na magonjwa ya aina hiyo waliendelea kutibiwa na kupona. Aliendelea kuingiza kiasi kikubwa cha fedha, utajiri wake ukazidi kuongezeka maradufu. Baada ya miaka mitano kupita, wakapata mtoto wa pili wa kike waliyempa jina la Cecilia. Latifa alikuwa na furaha tele, moyo wake ulikuwa na amani, hakuwa na kinyongo na mtu yeyote, maisha yake yalikuwa ya furaha tele. MWISHO…. *Nashukuruni sana kwa kuifuatilia simulizi hii. Mungu awabariki*

 Instagram Image by Shaaban Habibu🇹🇿🇰🇪🌹 (@storynzuriiplanet) with caption : "HADITHI:MREMBO LATIFA 98
MTUNZI:EDO MAN  Binti yangu! Ibrahim alinihadithia kila kitu kuhusu wewe hata kabla hajajua kam" at Dar es Salaam, Tanzania - 1975971641394973838

HADITHI:MREMBO LATIFA 98 MTUNZI:EDO MAN Binti yangu! Ibrahim alinihadithia kila kitu kuhusu wewe hata kabla hajajua kama mimi ni mzazi wako, naomba umsamehe, inawezekana mambo yote anayopitia, shida zote anazozipata ni kwa ajili ya laana yako, msamehe na sahau kila kitu,” alisema mzee Deo. Latifa akayapeleka tena macho yake kwa Ibrahim, alipanga kutokusamehe katika maisha yake lakini kila alipokuwa akimwangalia, bado mwanaume huyo alionekana kuhitaji msamaha. Alionekana kupigika katika maisha yake, alitia huruma lakini pamoja na hayo yote, alifanya kazi kubwa sana kumlea baba yake. Hakuwa na fedha za kutosha lakini nkiasi hichohicho kidogo alikitumia kwa ajili ya kumtibu baba yake, hakika alifganya jambo kubwa lililohitaji sifa kubwa kutoka kwake. Hakuongea kitu, alichokifanya ni kumsogelea na kumkumbatia. Wote wawili walikuwa wakibubujikwa na machozi. Latifa hakuwa na jinsi, aliukana moyo wake na kumsamehe mwanaume huyo aliyeonekana kuhitaji sana msamaha. “Nisamehe Latifa.” “Nimekusamehe Ibrahim, Ahsante kwa yote uliyomfanyia baba yangu,” alisema Latifa huku akijifuta machozi. “Naomba umsamehe Nusrat pia! Ni mwanamke mpumbavu asiyejua lile analolifanya. Naomba umsamehe.” “Nimsamehe Nusrat?” “Ndiyo! “Kwa hivi alivyomfanyia baba yangu? “Latifa! Hebu sahau kwanza. Wewe ni mtu mkubwa na mwenye heshima, tazama dunia nzima inakutazama wewe, usiposamehe, vipi wale vijana wanaotaka kuwa kama wewe? Nao watakapokosewa hawatakiwi kukosea kisa wewe haukusamehe? Vipi kuhusu wale watoto wanaotaka kuwa kama Latifa, kweli nao hawatakiwi kusamehe? Samahe saba mara sabini, au umesahau hilo?” aliuliza Ibrahim. “Nakumbuka.” “Basi naomba umsamehe!” “Nimemsamehe!” “Nashukuru!” Huo ndiyo ukawa mwanzo wa maisha mapya, Latifa hakuwa na kinyongo, moyo wake ulilainika na hakutaka kuwa na kingo na mtu yeyote yule, alichokiamua ni kumsahmehe kila mtu aliyewahi kumfanyia ubaya kwa makusudi au bahati mbaya. Alikuwa mtu mwenye mafanikio, bilionea, alichokifanya ni kumsafirisha baba yake nchini Marekani, alitaka akatibiwe huko na kuishi naye hukohuko. Kwa Ibrahim, japokuwa alimfanyia mambo mabaya nyuma hakutaka kumuacha hivihivi, aliamua kumsaidia kama alivyomsaidia baba yake.

 image by Shaaban Habibu🇹🇿🇰🇪🌹 (@storynzuriiplanet) with caption : "HADITHI:MREMBO LATIFA 97
MTUNZI:EDO MAN “Maisha, maisha yalinipiga na ndiyo maana nipo hivi,” alijibu mzee Deo.
Latifa a" - 1975969859100788029
ReportShareDownload057

HADITHI:MREMBO LATIFA 97 MTUNZI:EDO MAN “Maisha, maisha yalinipiga na ndiyo maana nipo hivi,” alijibu mzee Deo. Latifa akanyamaza, akamsogelea baba yake kitandani pale na kumbusu katika shavu la uso huku machozi ya furaha yakimbubujika mashavuni mwake. “Umefanana sana na mama yako,” alisema mzee Deo. “Nani? Mimi?” “Ndiyo! Mama yako alikuwa mrembo kama ulivyo,” alisema mzee Deo. “Sasa kwa nini ulimfukuza wakati alipokuwa na mimba yako?” “Nilimpenda sana mama yako, nilijitolea kwa kila kitu, nilitaka niishi naye japokuwa nyumbani kwao hawakuwa wakinipenda kisa tu nilikuwa mtu mweusi. Alipofukuzwa kwao, akakosa pa kwenda, alichoamua ni kuja nyumbani kwangu. “Hata kabla hajafika, tayari wazazi wake waliwatuma watu wawili, walikuja huku wakiwa na bunduki, waliniambia kwamba endapo ningempokea mama yako na kuishi naye, hakika wangeniua, na waliniambia kabisa kwamba walitumwa na wazazi wake,” alisema mzee Deo na kuendelea: “Niliogopa sana, niliona kweli ningeuawa, nilichokifanya ni kumfukuza Nahra huku nikiumia moyoni. Sikufanya vile kwa kuwa sikuwa nikimpenda, la hasha! Nilifanya vile kwa kuwa nyuma yangu niliwekewa bunduki. Alipoondoka, sikukaa nyumbani, niliondoka kwenda kumtafuta, usiku mzima nilimtafuta kila kona, ila sikufanikiwa kumpata, huo ukawa mwisho wa kuonana naye,” alisema mzee Deo, tayari naye machozi yalianza kumbubujika. Watu wote waliokuwa mahali pale walikuwa kimya wakimsikiliza, mzee huyo alitia huruma kitandani pale, alionekana kukosa nguvu na alikuwa mtu aliyekosa tumaini kabisa. “Nisamehe Latifa,” alisema mzee Deo. “Nimekusamehe baba! Kila kitu kilichopita, kimepita, ni lazima tugange yajayo,” alisema Latifa, hapohapo akayapeleka macho yake usoni mwa Ibrahim aliyekuwa kimya. “Ulimfahamu vipi Ibrahim?” “Ni mtu ambaye amenisaidia sana, bila yeye nafikiri leo hii nisingekutana na wewe. Alinionyeshea upendo mkubwa sana, sikuamini kama kuna watu wenye roho nzuri kama alivyokuwa yeye. Nimekuwa naye kipindi chote, nilipopata tatizo, alinisaidia kwa fedha kidogo aliyokuwa nayo. “Hakujua kama mimi ni baba yako, alinionyeshea upendo kwa kuwa aliona nastahili kufanyiwa hivyo japokuwa mke wake alikuwa ni tatizo kubwa.

 Instagram Image by Shaaban Habibu🇹🇿🇰🇪🌹 (@storynzuriiplanet) with caption : "HADITHI:MREMBO LATIFA 96
MTUNZI:EDO MAN 
Watu waliokuwa wamegundua kwamba msichana aliyekuwa mbele yao alikuwa Latifa wa" at Dar es Salaam, Tanzania - 1975966539577706925

HADITHI:MREMBO LATIFA 96 MTUNZI:EDO MAN Watu waliokuwa wamegundua kwamba msichana aliyekuwa mbele yao alikuwa Latifa walibaki wakishangaa, hawakuamini kama kweli yule aliyesimama mbele yao alikuwa ndiye au alikuwa msichana mwingine aliyefanana naye. “Inawezekana ndiyo yeye,” alisema jamaa mmoja huku akimwangalia Latifa ambaye machozi yalikuwa yakimbubujika tu. “Labda! Ila awe hapa anafanya nini?” “Sijui, hebu tusogee karibu zaidi tumuone.” Kila aliyepita, hakuacha kumshangaa Latifa aliyekuwa akilia tu. Ibrahim alikuwa kimya, moyo wake ulimuuma, alimzoea sana mzee Deo, alikuwa rafiki yake mkubwa, alimpenda pasipo kujua kwamba mzee huyo alikuwa mzazi wa msichana aliyemuacha kipindi cha nyuma, Latifa. Madaktari wakawa wanapishana mlangoni, wengine waliingia na wengine kutoka. Mgonjwa aliyeletwa kwao alionekana kuwa wa maana sana, ilikuwa ni bora kuleta utani kwa mgonjwa mwingine lakini baba yake Latifa. Baada ya msaa mawili, mlango ukafunguliwa na daktari kutoka, akawaita watu hao ofisini kwake kwa lengo la kuzungumza nao. Walipofika huko, akawaweka chini. “Hali ya mgonjwa si mbaya, alitoneshwa tu kidonda chake,” alisema Dk. Mimi, mwanamke mzuri mwenye umbo la kuvutia. “Ila ninataka kuzungumza naye, naweza kufanya hivyo?” “Hakuna tatizo, unaweza ila kama baada ya saa moja hivi, atahitaji muda wa kupumzika,” alisema Dk. Mimi. “Sawa!” Kusubiri halikuwa tatizo kabisa, alitaka kumsikia baba yake akizungumza kile alichokuwa akitaka kuzungumza. Alitaka kusikia kile ambacho hakuwa amekisikia kuhusu mama yake, kile alichosema Ibrahim kwamba mzee huyo alikuwa na la ziada. “Nyamaza Latifa,” alisema Dominick huku akimvuta Latifa upande wake. Walitulia kwa muda wa saa moja na ndipo walipoambiwa kwamba wangeweza kumuona mgonjwa wao. Wakainuka na kuingia ndani. Latifa alipomuona baba yake kitandani pale, uso wake ukajawa na tabasamu pana na kuanza kumsogelea. Moyo wake ukaingiwa na hisia kali, ukapatwa na furaha kubwa kiasi kwamba alishindwa kuliuia tabasamu lake kutawala usoni mwake. “Baba…” “Naam mwanangu.” “Nini kilitokea?” “Maisha, maisha yalinipiga na ndiyo maana nipo hivi,” alijibu mzee Deo.

 image by Shaaban Habibu🇹🇿🇰🇪🌹 (@storynzuriiplanet) with caption : "HADITHI:MREMBO LATIFA 95
MTUNZI:EDO MAN  walipolifungua geti dogo na kuingia ndani, wakamkuta Ibrahim akiwa amemshika mz" - 1975489887554973422
ReportShareDownload271

HADITHI:MREMBO LATIFA 95 MTUNZI:EDO MAN walipolifungua geti dogo na kuingia ndani, wakamkuta Ibrahim akiwa amemshika mzee Deo aliyekuwa chini huku akilia, mzee huyo alikuwa hoi, damu ziliendelea kumtoka katika kipande chake cha mguu na alikuwa akilia kwa maumivu makali. Wote wakamfuata, kila mtu aliyemwangalia, sura yake ilifanana na Latifa kwa mbali, hakukuwa na mtu aliyekuwa na ubishi kwamba mzee yule alikuwa mzazi wa Latifa. Latifa akajikuta akianza kulia, hasira ikamkaba kooni dhidi ya Nusrat, alionekana kuwa na hasira mno. “Hanijui, yaani pamoja na kuniumiza bado ananiumizia baba yangu! Atanitambua mimi ni nani,” alisema Latifa huku kwa kumwangalia tu ungegundua ni jinsi gani alikuwa na hasira. Walichokifanya ni kumchukua na kumpeleka hospitalini huku Latifa akiahidi kwamba ni lazima angemuonyesha Nusrat yeye alikuwa nani. **** Latifa alikuwa akilia tu, kila alipomwangalia baba yake, moyo wake ulimuuma mno, hakuamini kama alikuwa kwenye hali ile. Watu wengine walimbembeleza anyamaze lakini hakunyamaza, hasira kali dhidi ya Nusrat ilimkamata mpaka kufikia kiasi cha kukunya ngumi. Kitendo cha kupigwa baba yake na kuumizwa namna ile kulimuongezea hasira ya kumchukia Nusrat ambaye miaka michache nyuma alimuumiza kwa kumchukulia mwanaume wake, hakuonekana kuridhika, leo hii alimpigia baba yake. “Nitamuonyesha,” alisema Latifa huku akionekana kuwa na hasira kali. Hawakuchukua muda mrefu wakafika katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili. Japokuwa kipindi cha nyuma alisema kwamba baba yake alikuwa miongoni mwa watu aliokuwa akiwachukia kwa kuwa tu alkimfukuza mama yake lakini wakati alipokuwa akimwangalia, mateso aliyoyapata, chuki yote dhidi yake aliyokuwa nayo ikaondoka na huruma kumuingia. Manesi waliokuwa na machela wakasogea lilipokuwa gari lile na kumpajndisha mzee Deo juu ya machela ile na kuanza kusukumwa kwenda kwenye chumba kimoja kilichoandikwa Theatre. Walipofika nje ya chumba kile, wakazuiliwa. Watu waliokuwa wamegundua kwamba msichana aliyekuwa mbele yao alikuwa Latifa walibaki wakishangaa, hawakuamini kama kweli yule aliyesimama mbele yao alikuwa ndiye au alikuwa msichana mwingine aliyefanana naye.

 Instagram Image by Shaaban Habibu🇹🇿🇰🇪🌹 (@storynzuriiplanet) with caption : "HADITHI:MREMBO LATIFA 94
MTUNZI:EDO MAN “Latifa, huu ndiyo muda wa kuusikia ukweli, twende ukamuone baba yako, ameteseka" at Dar es Salaam, Tanzania - 1975487900990026540

HADITHI:MREMBO LATIFA 94 MTUNZI:EDO MAN “Latifa, huu ndiyo muda wa kuusikia ukweli, twende ukamuone baba yako, ameteseka sana, kansa ya mguu ilisababisha kukatwa mguu wake, twende ukamuone, atafurahi kama akikuona,” alisema Ibrahim. “Baba yangu……” alisema Latifa, sauti ya kilio chake ikaanza kusikika. “Ni kweli, yupo hai, hana pa kuishi, amekuwa akiteseka miaka yote, alikuwa ombaomba mitaani, alifukuzwa kila sehemu. Nimekuwa nikiishi naye kwa kipindi kirefu pasipo kujua kwamba ni baba yako, historia aliyonisimulia, ni hiyohiyo ambayo umesimulia japokuwa kuna kitu ambacho haukukifahamu, si wewe tu bali hata marehemu mama yako hakukifahamu, nimemsaidia sana mpaka kufikia kipindi hiki. Naomba twende ukamuone, tuwahi, namjua mke wangu, anaweza hata kumuua,” alisema Ibrahim. “Kumuua! Amuue baba yangu!” “Ni mwanamke mwenye roho mbaya! Twende Latifa,” alisema Ibrahim, hawakutaka kusubiri, waliposikia kwamba mke wa Ibrahim angeweza kumuua mzee Deo, wote wakaingia ndani ya gari na kuanza kuelekea huko. Garini, bado Ibrahim aliendelea kumuomba msamaha msichana huyo, alijutia matendo aliyoyafanya, hakuomba msamaha kwa kuwa Latifa alikuwa msichana bilionea, aliomba msamaha kwa kuwa alihitaji kusamehewa kwa yote aliyoyafanya. “Ibrahi…nime…kus…ame..he..” alisema Latifa huku akilia. Walichukua dakika kumi njiani ndipo walipofika alipokuwa akiishi Ibrahim. Kwa kuwa nyumba ilizungushiwa ukuta huku ikiwa na geti kubwa, Ibrahim akateremka na kwenda kulifungua geti lile ili gari liingizwe ndani. Kitu cha ajabu alipofika katika eneo la nyumba hiyo, akapiga uyowe mkubwa, mbele yake alikuwepo mzee Deo, alikuwa hoi chini, kama ilivyokuwa kipindi cha nyuma, muda huo napo damu zilikuwa zikimtoka katika kipande cha mguu wake, Nusrat alikuwa amemtoa ndani ya nyumba yake. Latifa na watu wengine waliposikia uyowe huo, wakahomoka kutoka garini, wakajua kwamba kulikuwa na kitu ndani ya nyumba hiyo, walipolifungua geti dogo na kuingia ndani, wakamkuta Ibrahim akiwa amemshika mzee Deo aliyekuwa chini huku akilia, mzee huyo alikuwa hoi, damu ziliendelea kumtoka katika kipande chake cha mguu

SPECIAL KWA WADADA: Umepata Bwana, Umempenda Kweli kweli na Umemlalamikia Sana Eti Kwanini Hakupeleki Kwa Wazazi Wake Kukutambulisha, Jamaa Akagoma Sana mwishowe akaona isiwe Kesi Akakupeleka Wewe badala hata utake hiyo advantage umefika tu Siku ya Kwanza Umeshinda Unachati, Siku ya Pili Umeshinda Unachati Tena ndio unajisifia kwenye groups 👌😏😏 upo ukweni Kumbe Wao Wanakutazama Tu na kukupimia Wala Hawakwambii Kitu Siku ya Tatu Wanakwambia Leo Ni Zamu Yako Kupika, Unaingia Jikoni unaona Kila Kitu Kigeni Vya Huku Unaweka Kule, Vya kule Unaweka Huku (Yaani Hujui Kupika Chochote 🤔🤔🤔) Sufuria Unashika Kama Umeshika Power Bank, Unapika Na Lipstick, Mdomo Mwekunduuu Utafikiri Mtoto wa Jini Katoka Kufundishwa Kunyonya Damu tena huku Umevaa Saa, Umevaa Culture Zimejaa Nusu Ya Mkono, Umevaa Mini Skirt Kama Wafanyakazi Wa Emirates Msosi wa Wakwe Huwezi Kupika������. Ukiambiwa Hufai Kuolewa Unavuta Mdomo Utafikiri Umenyimwa USB Cable Ubust Smartphone Yako Unaanza Kulalamika Wakwe Hawakupendi, Unalalamika Weee, Unashindwa Kuelewa Kuwa Wewe Ndo Tatizo. Usitake Kuolewa Ukidhani Mumeo Atakula Chips na Wewe Utakuwa Utakula Pizzas Kila Siku, Jifunze Hata Kuchemsha Chai Basi😂😂 Au Unadhani Google Wataleta App Ambayo Unaweka USB Kwenye Simu Yako Alafu Unaielekezea Kwenye Sahani Inaproduce Msosi JIPANGE DADA Usidhani Ndoa Ni Kama Kupiga selfie 👌 Utaishia kusema umelogwa kumbe we mwenyewe ndo mchawi😎💪 NIMEMALIZA🚶🚶 N:B; Kuelewa ni Mchakato Usipoelewa Leo utaelewa Mwakani..

LEO HII NDANI YA ACD (AFTER CLASS DISCUSSION) UTAKUWA NAE @kitalula AKIKULETE MADAA YA FASIHI UNAANZAJE KUKOSA NI NDANI YA @mtabeapp LIVE BILA CHENGA SAA 7 KAMILI MPAKA 8:30..

 image by Shaaban Habibu🇹🇿🇰🇪🌹 (@storynzuriiplanet) with caption : "HADITHI:MREMBO LATIFA 93
MTUNZI:EDO MAN 
Latifa hakuwa na kipindi kirefu katika kituo kile, alichokifanya Ibrahim ni kum" - 1975304173068280397
ReportShareDownload9120

HADITHI:MREMBO LATIFA 93 MTUNZI:EDO MAN Latifa hakuwa na kipindi kirefu katika kituo kile, alichokifanya Ibrahim ni kumwambia kwamba ilikuwa ni lazima kumfuata Latifa huko na kumwambia ukweli kwamba alikuwa na baba yake nyumbani kwake. “Ngoja nikamlete uzungumze naye,” alisema Latifa. “Atakubali kuja?” “Atakuja tu. Subiri,” alisema Ibrahim huku akionekana kuchanganyikiwa, hakutaka kuchelewa, akaondoka kuelekea huko, tena alikuwa akikimbia kwa kasi ajabu. Jina la Ibrahim lilimchanganya, hakuamini kama kweli aliitwa na msichana yule kwa kuwa alikuwa akihitajika na mtu aliyejitambulisha kwa jina hilo. Huku akionekana kuwa na hasira, akatoka pamoja na ndugu zake kuonana na huyo mtu. Alipofika, alipomwangalia Ibrahim, akajikuta akiingiwa na huruma, aliyesimama mbele yake alikuwa Ibrahim, yuleyule kijana aliyekuwa amemtesa na kumkataa kipindi cha nyuma, ila hali aliyokuwa nayo, ilimtia huruma mno. “Ibarhim,” alijikuta akimuita kijana huyo aliyeonekana kupigwa na maisha. “Latifa…” aliita Ibrahim, tayari machozi yakaanza kumbubujika, hata naye kumbukumbu za nyuma zikaanza kujirudia kichwani mwake. “Umefuata nini?” aliuliza Latifa huku akiwa amesiamam. “Kwanza naomba unisamehe kwa yote yaliyotokea, dunia imeniadhibu kwa kile nilichokufanyia,” alisema Ibrahim. Japokuwa alijiahidi kwamba asingeweza kumsamehe mwanaume huyo lakini hakuwa na jinsi, kwa namna ambavyo alionekana mahali hapo, ilionyesha kabisa kwamba maisha yalimpiga, hivyo hakutaka kumwadhibu tena, alichokifanya ni kuukunjua moyo wake na kumsamehe kwa kila kitu kilichotokea. “Nimekusamehe Ibrahim, dunia imekufunza,” alisema Latifa. “Kuna kitu ninahitaji kutoka kwako.” “Kitu gani?” “Baba yako anateseka Latifa, kila ulichoambiwa ni kweli kilitokea, ila naye ana historia ya tofauti na hiyo uliyokuwa nayo,” alisema Ibrahim, alikuwa amemsogelea kidogo, kila mtu akashtuka. “Baba yangu?” “Ndiyo!” “Nani?” “Mzee Deo!” “Hapana! Baba yangu kashakufa!” “Una uhakika? Ulionyeshewa kaburi lake? Au hata picha yake unayo” “Ibrahim, baba yangu! Haiwezekani!” “Latifa, huu ndiyo muda wa kuusikia ukweli, twende ukamuone baba yako, ameteseka sana, kansa ya mguu ilisababisha kukatwa mguu wake, twende ukamuone,

 Instagram Image by Shaaban Habibu🇹🇿🇰🇪🌹 (@storynzuriiplanet) with caption : "HADITHI:MREMBO LATIFA 92
MTUNZI:EDO MAN 
Ibrahim akamchukua mzee Deo na kwenda kutulia naye kochini, akachukua rimoti ya" at Dar es Salaam, Tanzania - 1975301072798282220

HADITHI:MREMBO LATIFA 92 MTUNZI:EDO MAN Ibrahim akamchukua mzee Deo na kwenda kutulia naye kochini, akachukua rimoti ya televisheni na kisha kuiawasha. Mzee Deo alikaa kitini, hakujisikia kuangalia, hakuwa na amani kabisa kwani jinsi alivyokuwa akimwangalia Nusrat ambaye alikaa pembeni kabisa, alionekana kuwa na hasira mno. Latifa alivyoonyeshwa kwenye televisheni, Ibrahim akajikuta akianza kububujikwa na machozi, moyo wake uliumia, kila alipokuwa akimwangalia msichana yule, akagundua kwamba aliitupa almasi jangwani na kuokota bati. Msichana huyo mrembo, mwenye muonekano wa fedha akaanza kusimulia historia ya maisha yake. Kila mmoja akabaki kimya akimsikiliza, alianza kusimulia kuanzia mbali, tangu mama yake alipofukuzwa nyumbani kwao, alipokwenda nyumbani kwa mpenzi wake, Deo kisha kumfukuza, alionekana kuumia mno. Mzee Deo aliposikia historia aliyokuwa akiisimulia Latifa, akashtuka, akaanza kumwangalia Latifa, akasimama kutoka katika kochi lile na kuisogelea televisheni, kila mmoja mule ndani akabaki akimshangaa. “Ibrahim….” aliita mzee Deo, machozi yakaanza kumtoka. “Nipo mzee….” “Latifa ni binti yangu!” alisema mzee Deo huku akionekana kushangaa, Ibrahim akashtuka, si yeye tu, hata Nusratakashtuka. “Unasemaje?” “Kumbe Latifa ndiye mtoto wangu aliyezaliwa na Nahra,” alisema mzee Deo. Hapo ndipo Ibrahim alipoanza kukumbuka mahojiano yale, alikumbuka Latifa alimtaja mtu aliyeitwa Nahra na Deo, wazazi wake waliokuwa kwenye mahusiano ya kimapenzi mpaka baba yake alipomfukuza mama yake. Mahojiano yale akayaunganisha na historia aliyowahi kusimuliwa na mzee huyo kwamba zamani alikuwa na mwanamke wa Kihindi, alimpa ujauzito lakini baadaye akafukuzwa nyumbani kwao, na alipokuja kwake, naye alimfukuza ila ni kwa sababu tu alitishiwa kuuawa na ndugu zake Nahra kwa kutumiwa watu waliokuwa na bunduki, na kama asingemfukuza basi angeuawa yeye. “Ni mtoto wangu! Kumbe Latifa ni mtoto wangu!” alisema mzee Deo huku akijifuta machozi. Ibrahim alishindwa kuamini, wakati mwingine alifikiri kwamba alikuwa ndotoni, katika kipindi chote alichokuwa akiishi na huyo mzee, alivyokuwa akizungumza naye kumbe alikuwa mzazi wa msichana aliyekuwa amemuacha, Latifa.